PASKA NJEMA

nsimambotend02.jpg

Amefufuka, kama alivyosema, Aleluya!    - Siku kuu ya Paska (TOA) – 24 avril 2011  

Enjili ya Mateo : 28,1-8 Baada ya sabato, kulipoanza kumulika siku ya kwanza ya juma. Maria Magdalena na yule Maria mwingine walikuja kuliangalia kaburi. Mara kukawa mtetemeko mkubwa wa nchi, maana Malaika wa Bwana alishuka toka mbinguni, akaja kuliviringisha lile jiwe, akaketi juu yake. Sura yake ilikuwa kama umeme, na mawazi yake meupe kama zeluji. Walinzi wakatetemeka sababu ya kuogopa, wakawa kama wafu. Malaika akawambia wale wanawake: “ Ninyi musiogope: maana najua kama mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. Hayupo hapa, maana amefufuka, kama alivyosema, Njooni, mtazame mahali Bwana alipokuwa amelala. Tena nendeni upesi, mkawambie wafyasi wake: Amefufuka katika wafu! Tazameni, anawantangulia ninyi kwenda Galilea, huko mtamwona. Haya, ninawapashaninyi neno hilo. Nao wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha kubwa, wakapiga mbio kuwapasha wafuasi wake habari.

 

Wandugu, tusitupilie mbali akili zetu. Mungu, alituumba na akili na kutupatia uwezo wa kutumia akili zetu ili tuweze kufikiri na kuvumbua vitu mbali mbali. 

Lakini tunajua kama hutuwezi kuvumbua yote, na mara mingi tunakuta njiani ya maisha yetu ya kila siku mambo mengi yenyi kubakiliwa bila jibu, wala   yaliyojifichwa na siri ao na fumbo.   Kufuatana na nyakati tunazokuwemo sisi watu tunapenda zaidi kujua wazi vitu vyote. Lakini si vile, kwani mara mingi tunaona kama hatuwezi, hatusikie, hatutambue, japo wenyi akili tunapenda kujua wazi vitu vyote.   

Lakini hatuwezi kujua yote, na tunajikuta kabisa na uzaifu wa maisha yetu ya wanadamu.  Leo tuko na mambo mengi katika maisha, tunajikaza kujua na kufumbua mambo haya yote, lakini mara mingi tunashindwa. Na tunajisikia bila uwezo. Ni vile mbele ya mambo ya ajabu ya ufufuko wa Bwana. Hatuwezi kuona yote na macho yetu, hatuwezi kujua vyote na akili, lakini tunasaidiwa kabisa na imani. Watakatifu wanatuambia: Mukitaka kujua kabisa mambo ya Mungu, mukipenda kuvumbua fumbo la Mungu, ujikaze kupiga magoti, tia moyo yako mikononi mwake, na husiseme kitu… ngoja tu yeye aseme.” 

Mara kukawa mtetemeko mkubwa wa nchi, maana Malaika wa Bwana alishuka toka mbinguni, akaja kuliviringisha lile jiwe, akaketi juu yake” Mtetemeko wa nchi, wa udongo, wa manyumba… ilisikilizwa…mtetemeko ya Ufufuko… Leo siku ya Paska tunafika sisi pia, pamoja na Maria Magdalena na yule Maria mwingine kuliangalia kaburi, kumtafuta yule tuliloacha kaburini siku ya tano mangaribi. Tunafika kaburini na hali ya wale wanawake. Tunafika kwa kulia machozi mbele ya lile jiwe mkubwa linayeficha ndani mwili ya yule mpenzi wetu.  Kama vile wale wanawake sisi pia tunajazwa na woga, tuko na wasiwasi, tunangahika sana.  

Leo na kinywa cha malaika, kama vile wimbo wa Noeli wa malaika mbinguni, asema: “ Ninyi musiogope: maana najua kama mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. Hayupo hapa, maana amefufuka, kama alivyosema, Njooni, mtazame mahali Bwana alipokuwa amelala. Tena nendeni upesi, mkawambie wafyasi wake: Amefufuka katika wafu! Tazameni, anawantangulia ninyi kwenda Galilea, huko mtamwona.” Mtakatifu Augustino anatuambia: Sisi wakristu ni watu wa Paska na wimbo wetu ni Aleluya”.  Sisi wakristu ni watu wa “kupita” (paska, maana yake mapito), Sisi wakristu ni watu wa Aleluya (maana yake Mumsifu Mungu Yahwe). Kupita ndiyo kutoha katika hali ya ubaya, ya zambi, na fufua wema, fufua upendo, fufua imani yako, fufua matumaini.  

FUFUA WEMA: wema hauozi!
FUFUA UPENDO, kwani  Kufufuka kwa Yesu ni kufuka kwa upendo. Ukiutoa upendo, dunia inakuwa kama kaburi, jamaa  inakuwa kama kaburi, nchi inakuwa kama kaburi.  Katika maisha tunaweza kuwasaidia wengine bila kuwapenda lakini hauwezi kupenda bila kusaidia bila kuwa mkarimu. “Mbolea haileti faida ikiwa katika lundo kubwa, lakini inaposambazwa inafanya maajabu.”
FUFUA IMANI YAKO. Ni ya lazima zaidi kwa siku za leo, katika nchi yetu, na duniani kote. Pato ya maisha ya watu wengi ni mbali ya dini, ya Mungu,  ya imani. Watu wengi wameua imani yako kwa Mungu, aasema: dini ni dini.  Imani yako ifufuke.
Hakuna milango ambayo itafunguliwa bila imani. Imani yako iwe usukani na isiwe kama tairi
la akiba. Ukifikiria kukamata panya hauwezi kukamata simba. Imani ni kama mswaki lazima uwe na wako.
FUFUA MATUMAINI: Paska inaleta upya duniani kote. Paska inaleta upya katika nchi, katika jamaa, katika makanisa zetu. Moto huteketeza nyasi lakini hauchomi mizizi. Walipomuua Yesu waliteketeza nyasi lakini hawakuteketeza mizizi ya uwezo wake wa kufufuka. Tuuze matumaini. Nidyo ndoto ya kujenga ubora na usawa wa nchi, wa jamaa, wa kanisa, wa serkali, wa jamii mzima… Fufua matumaini, ndiyo kujweka wima, kuonyesha uhuru wetu. Sifa ya Mungu, ni mtu wima, alikuwa kusema Mtakatifu Ireneo.  
Usiogope. Tosha woga. Tosha usingizi.  Ujikaze kupigana na maovu yote. Usafishe, uanze kulima… Kwani tangu siku Paska Yesu atakuwa pamoja na sisi, kwani yeye ni mzima kati yetu… Mwanzoni Maria Magdalena hakuona mazingira ya matumaini. Aliona jiwe limeondolewa kaburini, bila kumwoha malaika.  Aliwaza kuwa askari wameendelea kuadhibu mwili wa marehemu na  wamemutoa kwenda kuufanyia maovu zaidi,  au waibaji miili ya marehemu wameuiba. Macho ya Maria Magdalena hayakuona mazingira ya matumaini. 

Musiogope hamutakwa wayatima, mimi niko pamoja nanyi siku zote… Maria Madgalena alikuwa ameenda kuupaka mwili wa Yesu manukato. Alienda kumtafuta Yesu katika wafu. Maria Madgalena alienda kumtafuta Yesu aliyesulubiwa. Lakini Yule Yesu aliyesululiwa alikufa. Mungu wetu ni Mungu wa wazima, sio wa wafu. Mungu anayekufa si Mungu tena:  yule malaika akawaambia wale wanawake, ‘Nyinyi msiogope! Najua kwamba mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa.” (Mathayo 28: 5) 

Musiogope, Amefufuka, Tazameni, Nendeni kuwapasha habari hizoMaria Magdalena aliona na macho ya upendo. Alikumbuka maneno zote za Yesu,  hakuingia kaburini… aliitika, alipiga mbio kwenda kupasha habari ya furaha ya Paska kwa wafuasi.  Tuone na macho ya mwili na kuona na macho ya imani zaidi macho yetu ya imani ifunguliwe na macho ya upendo.  Mungu wetu ni wa kutimiza ahadi. Yesu alisema naweza kulibomoa hekalu nikalijenga siku tatu alibomoa na kulijenga. Siku ya tatu alifufuka. Pasaka inatutaka tuwe wafanya biashara wa matumaini ua upendo. Ndiyo wamissionari wa Paska.  

Kwa kumaliza. 

Ili kufufuka ondoa jiwe. Fungua kabisa kaburi chako, uingize ndani mwangaza na moto ya Paska.  Jiwe kuko ndani ya uwezo wetu, ya mataa yetu, ya uyanguyangu wetu. Jiwe huko ndani ya kiburi, ya vita, ya magonvi, ya ulevi, ya wizi, ya kupigana. Jiwe huko ndani  ya kukosa amani, uhaki, heshima, ndani ya uwongo wa kila haina.

Ili kufufuka toka Kaburini
Mungu anakuita. Kaburi lina giza. Labda tupo ambapo kuna giza tunahitaji kuja kwenye mwanga. Labda umekata tamaa toka nje. Uwe na uhodari, na usiogope tena.
 

Leo ni leo, liwezekanalo leo lisingoje kesho. Matumaini ni yako yahimarishe. Jana ni yako ikufundishe. Leo ni yako timiza ndoto zako. Kesho ni yako tegemea mazuri. Ukabila upo umalize. Udini upo utupilie mbali. Watu ni wako wapende. Ukweli ni wako, ujue. Ugonjwa unaokusumbua upatie kwa heri ya kutoonana Maisha ni yako yaongeze. Ushindi ni wako jitwalie. Usiogopeshwe na kitu chochote umeumbwa katika mfano na sura ya mwenyezi Mungu.Ee Yesu, mfufuka wa wafu,  kama niko kinyogo, unidondoshe. Kama nataka kulipiza kisasi, unisamehe. Kama niko na kishawishi, unisaidie kishinde. Kama niko na chuki unipanguse. Kama niko na uchungu ukung’ute. Kama una kilema, nenda juu yake. Kama hakuna mapatano patana. Kama unafitina moyoni, ifukuze. Kama una mlima wa matatizo uondoe kwa imani. Kama una ubaya, ushinde kwa wema. Kama kifo kinakuogopesha kicheleweshe. Kama una msalaba, ubebe. Kama una changamoto, ikabili. Ee Yesu mfufuka, Wakikuangusha inuka. Wakikucheka wape tabasamu. Wakikusema vibaya, waombee. Wakikuchukia wapende. Wakikuua fufuka. Ee Yesu mfufuka unisaidie na unipatie nguvu na uhodari. Amen. 

Paska njema kwa kila mmoja na katina nchi yetu ya Kongo.     © Kakaluigi, Paska 2011 (24 avril 2011)  

Pas encore de commentaire.

Laisser un commentaire

"DIEU NOUS EST PROCHE&... |
Pourquoi suis-je sur terre |
la confrerie des playdébils |
Unblog.fr | Annuaire | Signaler un abus | voyance et cartomancie
| Eclairage Evangélique
| Rackam